Aug 05, 2020 11:00 UTC
  • Iran yatuma misaada ya chakula na dawa Lebanon

Hilali Nyekundu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetuma shehena ya kwanza ya misaada ya dharura ya dawa, vifaa vya tiba na chakula nchini Lebanon kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa mlipuko wa jana mjini Beirut.

Msemaji wa Hilali Nyekundu ya Iran Mohammad Nasiri amesema kufuatia mlipuko huo wa Beirut, Hilali Nyekundu ya Iran inatuma misaada yenye uzito wa tani tisa. Aidha amesema Hilali Nyekundu ya Iran itafungua hospitali ya muda na kutuma timu ya madaktari na wahudumu wa afya 22 Lebanon katika awamu ya kwanza. Amesema misaada hiyo inatumwa kufuatia ombi la mkuu wa Hilali Nyekundu ya Lebanon George Kataneh.

Mlipuko ya jana Beirut

Idadi ya watu waliouawa kwenye mripuko mkubwa katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut, imepindukia 100, huku wengine 4,000 wakiwa wamejeruhiwa. Bado haijafahamika kilichosababisha mripuko huo, hata hivyo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Lebanon, Mohammed Fahmi, amesema huenda shehena kubwa ya kemikali ya ammonium nitrate kwenye bandari ya Beirut iliripuka. 

Tags

Maoni