Aug 11, 2020 01:28 UTC
  • Kabila la Akidat la nchini Syria laanzisha muqawama dhidi ya vikosi vya Marekani na wanamgambo wa SDF

Kabila la Akidat katika mkoa wa Deir- ez Zor nchini Syria limeanzisha muqawama wa wananchi dhidi ya wanajeshi wa Marekani na waitifaki wao.

Kabila hilo limewatuhumu pia wanamgambo kwa jina la vikosi vya Kidemokrasia vya Syria (SDF) kuwa vinaiba maliasili za nchi hiyo.

Gazeti la al Rai al Youm lenye makao yake Marekani limeeleza katika tovuti yake kuwa, kabila la Akidat limetangaza kuunda baraza la kijeshi na kuanzisha muqawama wa wananchi dhidi ya wanajeshi wa Marekani na wanamgambo waitifaki wa Washington. Kabila hilo aidha limewatuhumu wanajeshi wa Marekani kuwa wamehusika na mauaji ya Matshar al Hafl, mwakilishi wa ngazi ya juu wa kabila hilo.

Taarifa iliyotolewa na kabila hilo la Akidat katika mkoa wa Deir ez Zor huko Syria imevituhumu pia vikosi vya SDF kuwa vinaiba maliasili za nchi hiyo na kuwauwa watu mashuhuri.

Vikosi vya SDF nchini Syria  

Wakati huo huo wazee na wawakilishi watajika wa kabila hilo wamefanya mkutano ili kuchukua hatua dhidi ya wanajeshi vamizi wa Marekani na mamluki wanaoungwa mkono na nchi hiyo kwa lengo la kuikomboa ardhi ya Syria.   

Katika mkutano wao huo, wawakilishi hao wa kabila la Akidat wamekubaliana kuunda baraza la kisiasa na jeshi la kikabila kwa ajili ya kusimamia masuala ya kabila hilo kwa ushirikiano na mamlaka husika.

 

Tags

Maoni