Aug 17, 2020 13:14 UTC
  • Msafara wa silaha na zana za kijeshi za Marekani kutoka Kuwait waingia Basra, Iraq

Duru moja ya masuala ya usalama ya Iraq imeripoti kuwa, msafara wa malori ya kijeshi ya Marekani yaliyosheheni silaha na zana nyingi za kijeshi umeingia katika ardhi ya nchi hiyo kwa lengo la kuhamishia silaha na zana hizo katika kituo cha kijeshi cha Ainul-Asad.

Kwa mujibu wa duru hiyo, msafara huo wa malori ya kijeshi ya Marekani yaliyosheheni zana na silaha za kivita ambao umetokea Kuwait, umepitia mkoani Basra ukielekea kituo cha anga cha Ainul-Asad kilichoko katika mkoa wa Al-Anbar magharibi mwa Iraq.

Sambamba na kuingia msafara huo wa kijeshi katika ardhi ya Iraq hapo jana, ndege za kivita za Marekani zilipaa katika anga ya nchi hiyo ili kuulinda msafara huo na kuusindikiza hadi kwenye kituo cha kijeshi cha Ainul-Asad.

Askari wa jeshi la kigaidi la Marekani katika mitaa ya ardhi ya Iraq 

Mashirika yanayohusika na masuala ya usalama ya Marekani ndiyo yaliyokadhibiwa jukumu la kuhamishia zana na silaha hizo kwenye kituo cha Ainu-Asad, wakati askari wa jeshi la kigaidi la Marekani wanatazamiwa kuhamishiwa kwenye kituo hicho cha anga na maeneo mengine walikowekwa askari wa Marekani kwa kutumia ndege za kivita za nchi hiyo.

Washington imechukua hatua hiyo ya kuhamishia nchini Iraq shehena kubwa ya silaha na zana za kijeshi ilhali mnamo tarehe 5 Januari 2020 wabunge wa Iraq walipitisha mswada wa kutaka vikosi vya jeshi vamizi la Marekani viondoke katika ardhi ya nchi hiyo.../ 

Tags