Sep 01, 2020 07:44 UTC
  • Ngao ya makombora ya Syria yazima mashambulizi ya anga ya  Israel

Jeshi la Syria limetangaza kuwa, mfumo wake wa ulinzi wa anga umefanikiwa kutungua makombora ya utawala wa Kizayuni wa Israel kusini mwa mji mkuu wa nchi hiyo ya Kiarabu, Damascus.

Shirika rasmi la habari la Syria SANA limeripoti kuwa, ngao hiyo ya makombora ya Syria imetungua akthari ya makombora ya utawala haramu wa Israel kabla hayajapiga shabaha.

Duru za kijeshi zimeiambia SANA kuwa, maadui wa Kizayuni walifanya hujuma hiyo ya anga jana Jumatatu tokea kwenye Miinuko ya Golan ya Syria na kulenga maeneo ya kijeshi kusini mwa Damascus.

Habari zaidi zinasema kuwa, wanajeshi wawili wa Syria wameuawa shahidi katika hujuma hiyo ya Wazayuni, mbali na wengne saba kujeruhiwa.

US na Israel zimekuwa zikitekeleza hujuma za anga dhidi ya Syria mara kwa mara

Mbali na chokochoko hizo za Israe, lakini hadi sasa nyumba nyingi za raia wa Syria zimebomolewa na miundo mbinu kuharibiwa pia huko mashariki mwa Syria kutokana na mashambulizi mtawalia ya muungano huo vamizi unaoongozwa na Marekani. 

Taasisi za kimataifa zimefumbia macho ombi la serikali ya Damascus la kutaka kusimamishwa haraka iwezekanavyo mashambulizi hayo ya muungano eti wa kupambana na ugaidi unaoongozwa na Marekani ambayo yamepelekea kuuliwa na kujeruhiwa makumi ya raia wa Syria. 

Tags

Maoni