Sep 15, 2020 07:28 UTC
  • Palestina: Jumanne ni 'Siku Nyeusi' kwa ulimwengu wa Kiarabu

Waziri Mkuu wa Palestina amesema ulimwengu wa Kiarabu leo Jumanne utashuhudia 'Siku Nyeusi' katika historia yake, kutokana na hafla itakayofanyika hii leo katika Ikulu ya White House ya Marekani ya kutiwa saini rasmi makubaliano ya kufanywa wa kawaida uhusiano wa nchi mbili za Kiarabu na utawala haramu wa Israel.

Mohammad Shtayyeh sanjari na kulaani hatua ya Bahrain ya Ijumaa iliyopita na Umoja wa Falme za Kiarabu Agosti 13 ya kutangaza kuanzisha uhisiano wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni, amesema historia ya ulimwengu wa Kiarabu hii leo itanakili tukio chungu na la kuumiza.

Shtayyeh amesema:Kesho (leo Jumanne) tutashuhudia siku nyeusi katika historia ya uliwengu wa Kiarabu na kufeli taasisi za Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) ambazo zina mgawanyiko. Hii itakuwa tarehe nyingine ya kuongezea katika kalenda ya matukio chungu ya Palestina.

Watawala wa Imarati na Bahrain kuwaangukia miguuni Netanyahu(kulia) na Trump katika Ikulu ya White House

Waziri Mkuu wa Palestina amesema Mamlaka ya Ndani ya nchi hiyo ya Kiarabu inapaswa kutazama upya uhusiano wake na Arab League, kutokana na jumuiya hiyo ya kieneo kushindwa kuzuia kufikiwa mapatano hayo na Wazayuni.

Mamlaka ya Ndani ya Palestina imetoa mwito wa kufanyika maandamano leo Jumanne, kulaani usaliti huo wa watawala wa Imarati na Bahrain. Kadhalika imeyataka mataifa mengine ya Kiarabu yasihudhurie hafla ya kusaini makubaliano hayo hii leo katika ikulu ya White House.

Tags

Maoni