Sep 22, 2020 02:37 UTC
  • Sheikh Ekrima Sa'id Sabri
    Sheikh Ekrima Sa'id Sabri

Khatibu wa Msikiti wa al Aqswa ambaye pia ni Rais wa Kamati Kuu ya Kiislamu ya Mji wa Quds (Jerusalem) amesema kuwa ni haramu kwa Waislamu kuimba wimbo wa taifa wa Israel.

Sheikh Ekrima Sa'id Sabri amesema kuwa "wimbo wa taifa" wa Israel una vipengee vinavyodai kuwa Wazayuni ni wamiliki wa ardhi za Palestina, mji wa Quds na Msikiti wa al Aqswa ambao ni sehemu ya tatu takatifu zaidi ya Kiislamu. Sheikh Sabri ameyasema haya akijibu hatua ya Waimarati ya kuimba wimbo huo. 

Msikiti mtukufu wa al Aqsa  

Sheikh Sabri amesema kuwa, baadhi ya watu nchini Imarati wanauimba wimbo wa taifa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa sababu ya ujinga wao au kwa kuwafuata Wazayuni. 

Katika wiki za karibuni na baada ya kuanzishwa uhusiano rasmi kati ya Imarati na utawala wa Kizayuni wa Israel, kulisambazwa picha ya video katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha raia mmoja wa Imarati akiimba wimbo huo wa utawala wa Kizayuni; hatua iliyopongezwa na utawala huo. 

Msemaji wa Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, amekaribisha kitendo hicho cha raia wa Imarati.    

Tags

Maoni