Sep 24, 2020 07:09 UTC
  • Shambulizi la kombora la Yemen dhidi ya kambi ya kijeshi ya Saudia laua 10

Jeshi la Yemen likishirikiana na vikosi vya kujitolea vya wananchi limetekeleza shambulizi la ulipizaji kisasi dhidi ya kambi ya kijeshi ya Saudi Arabia na kuua kwa uchache watu 10.

Kanali ya televisheni ya al-Jazeera ya Qatar imeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, shambulizi hilo la kombora la usiku wa kuamkia leo limelenga kambi ya kijeshi ya mamluki wa Saudia katika mkoa wa Saada ulioko karibu na eneo la Dhahran, katika mpaka wa kusini wa Saudia.

Jeshi la Yemen na vikosi vya kujitolea wananchi wa Yemen havijatoa taarifa kuhusiana na shambulizi hilo la kombora, lakini duru za habari zinaarifu kuwa, hujuma hiyo ya ulipizaji kisasi imelenga vikosi tiifu kwa kwa rais mtoro wa Yemen aliyejiuzulu na kukimbilia Riyadh, Abdu Rabbu Mansur Hadi.

Vikosi vya kujitolea wananchi vya Yemen

Mapema mwezi huu pia, harakati ya Ansarullah ya Yemen ililenga kwa kombora la balestiki na ndege zisizo na rubani (droni) maeneo kadhaa ya kistratajia ndani ya mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh.

Vikosi vya Yemen vimekuwa vikisisitiza kuwa, vitaendelea kutoa majibu makali zaidi dhidi ya Saudi Arabia iwapo muungano vamizi unaoongozwa na utawala wa Aal-Saud hautasitisha uvamizi wake, mzingiro na mauaji dhidi ya wananchi wa Yemen unaoyafanya tokea Machi 2015.

Maoni