Sep 24, 2020 11:59 UTC
  • HAMAS: Mpango wa Israel wa kupora ardhi za Ukingo wa Magharibi utagonga mwamba

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, njama za Marekani na utawala haramu wa Israel za kutaka kutwaa ardhi zaidi katika Ukingo wa Magharibi na kuziunganisha na ardhi nyingine zilizoghusubiwa za Palestina zitashindwa na kugonga ukuta.

Hazim Qassim amesema kuwa, matamshi ya balozi wa Marekani huko Israel  kuhusiana na mpango wa kutwaa ardhi ya Palestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan  kuziunganisha na ardhi nyingine zilizoghusubiwa za Palestina ni ishara ya wazi ya kiwango cha ufahamu usio sahihi aliona.

Kiongozi huyo wa Hamas amesema, Wapalestina wamesimama kidete na wataendeleza harakati na mapambano yao dhidi ya mipango yoyote inayolenga kupora haki za Wapalestina kama uporaji wa ardhi zao.

David Friedman, balozi wa Marekani huko Israel alitangaza hivi karibuni kwamba, utekelezwaji wa  mpango wa utawala haramu wa Israel wa kutaka kutwaa asilimia 30 ya eneo la Palestina la Ukingo wa Magharibi na kuliunganisha na ardhi nyingine zilizoghusubiwa za Palestina, umesitishwa kwa muda tu na kwamba, haujafutwa moja kwa moja.

Wanapambano shupavu wa Hamas

 

Mwezi Aprili mwaka huu, Benjamin Netanyahu, kiongozi wa chama cha Likud na Benny Gantz kiongozi wa chama cha Blu na Nyeupe, walifikia makubaliano ya kutwaa asilimia 30 ya eneo la Palestina la Ukingo wa Magharibi na kuliunganisha na ardhi nyingine zilizoghusubiwa za Palestina.

Mpango huo ulipangwa kuanza kutekelezwa kuanzia tarehe Mosi Julai mwaka huu lakini ulieakhirishwa baada ya kuongezeka mashinikizo na malalamiko ndani na nje ya Palestina dhidi ya mpango huo.

Tags

Maoni