Sep 24, 2020 11:59 UTC
  • Walebanon waandamana dhidi ya hatua ya Imarati na Bahrain ya kuanzisha uhusiano na Israel

Maelfu ya wananchi wa Lebanon wameandamana katika mji mkuu Beirut na kutangaza upinzani wao dhidi ya hatua yoyote ile ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.

Waandamanaji hao wenye hasiwa wakiwa wamebeba mabango na maberamu wamesikika wakipiga nara za kulaani hatua ya mataifa mawili ya Kiarabu ya Imarati na Bahrain ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Waandamanaji hao ambao walikuwa wamebeba pia bendera za Palestina wametangaza pia mshikamano wao na wananchi madhlumu wa Palestina ambao ardhi zao zinaendelea kuporwa na haki zao kughusubiwa kila leo na utawala dhalimu wa Israel.

Baadhi ya wanaandamanaji hao walichoma moto bendera ya utawala vamizi wa Israel na kutoa wito kwa wapenda haki ulimwenguni kuwa pamoja na wananchi wa Palestina.

Mwishoni mwa maandamano yao, waandamanaji hao walikusanyika mbele ya jengo la ubalozi wa Imarati mjini Beirut na kupiga nara dhidi ya viongozi wa Abu Dhabi.

Hafla ya utilianaji saini tawala za Imarati na Bahrain kwa ajili ya kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel

 

Hivi karibuni Mawaziri wa mashauri ya Kigeni wa Imarati na Bahrain walijipeleka kwa Donald Trump huko Marekani na kutia saini hati za kutangaza kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel kinyume kabisa na malengo ya wananchi wa Palestina.

Hadi hivi sasa ulimwengu mzima wa Kiislamu bali hata baadhi ya nchi zisizo za Waislamu, kama Afrika Kusini zinalaani kitendo hicho cha kisaliti cha Bahrain na Imarati.

Tags