Sep 25, 2020 02:33 UTC
  • Imarati yafanya biashara na mashirika ya Kizayuni yaliyoko kwenye orodha nyeusi ya UN

Mashirika kadhaa ya Umoja wa Falme za Kiarabu UAE yamesaini mkataba wa ushirikiano na mashirika na makampuni ya Kizayuni yaliyoko kwenye orodha nyeusi ya Umoja wa Mataifa kwa kuunga mkono ujenzi haramu wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni.

Vyombo rasmi vya habari vya Imarati vimetangaza kuwa benki ya Leumi ya Israel, ambayo iko kwenye orodha nyeusi ya Umoja wa Mataifa kutokana na kuunga mkono ujenzi haramu wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina inayokaliwa kwa mabavu imesaini mikataba mitatu ya ushirikiano na benki tatu za Imarati.

Mashirika ya Imarati yamesaini pia hati za maelewano na benki ya Kizayuni ya Hapoalim, ambayo nayo pia iko kwenye orodha nyeusi ya Umoja wa Mataifa.

Hatua ya mashirika ya Umoja wa Falme za Kiarabu ya kusaini mikataba ya ushirikiano na mashirika na makampuni ya Kizayuni yanayounga mkono ujenzi wa vitongoji hayajakomea katika mabenki ya utawala huo tu kwani kamati ya filamu ya Abu Dhabi imetangaza kuwa imesaini mkataba wa ushirikiano na mfuko wa sinema wa Israel na kituo cha uzalishaji athari za sinema cha Sam Spiegel kilichoko Quds tukufu inayokaliwa kwa mabau.

Bin Zayed na Netanyahu

Baada ya Imarati na Bahrain kutangaza uamuzi wa kiuhaini na usaliti wa kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni, tarehe 15 Septemba, nchi hizo mbili ndogo za Kiarabu za eneo la Ghuba ya Uajemi zilisaini rasmi mikataba ya kuanzisha uhusiano huo wa kidiplomasia na kuutambua rasmi utawala bandia wa Israel katika hafla iliyofanyika Ikulu ya White House na kuhudhuriwa na rais wa Marekani Donald Trump na waziri mkuu wa utawala huo wa Kizayuni Benjamin Netanyahu.../ 

Tags

Maoni