Sep 26, 2020 07:51 UTC
  • Pompeo atishia kufunga ubalozi wa Marekani nchini Iraq endapo utaendelea kushambuliwa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo ametoa vitisho kwa viongozi wa Iraq kwamba Washington inaweza kuamua kuufunga ubalozi wake ulioko mjini Baghdad.

Gazeti la Washington Post limeripoti kuwa Pompeo amewatishia viongozi wa Iraq kwamba Marekani inaweza ikaamua kufunga ubalozi wake ulioko nchini humo ikiwa utaendelea kushambuliwa.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, Rais Barham Salih wa Iraq siku ya Jumatatu iliyopita alitangaza katika kikao na viongozi wa makundi mbali mbali ya kisiasa ya nchi hiyo kwamba, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo amemuonya kuwa, ikiwa hujuma na mashambulio dhidi ya ubalozi na askari wa nchi hiyo walioko nchini Iraq vitaendelea, Washington itafunga ubalozi wake wa mjini Baghdad.

Rais Barham Salih wa Iraq

Pompeo amesisitiza kuwa Rais Donald Trump wa Marekani anaendelea kuchunguza kwa uzito mkubwa wazo la kuufunga ubalozi wa Marekani mjini Baghdad.

Katika miezi ya karibuni, ubalozi wa Marekani katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad, misafara ya kijeshi na vituo vya askari wa jeshi la kigaidi la nchi hiyo vilivyoko nchini humo vimeandamwa na mashambulio kadhaa.

Wananchi wengi wa Iraq pamoja na makundi na mirengo ya kisiasa na kidini ya nchi hiyo wanataka askari wa jeshi la kigaidi la Marekani waondoke nchini humo; na hata bunge la nchi hiyo limeshapitisha mpango wa kutaka askari hao waondoke katika ardhi ya Iraq.../

Tags

Maoni