Oct 18, 2020 04:25 UTC
  • Serikali ya Yemen: Tunashikilia mateka maelfu ya mamluki wa Saudia na Sudan

Kamati ya Taifa inayoshughulikia masuala ya matekani nchini Yemen imetangaza kuwa jeshi la nchi hiyo linawashikilia mateka maelfu ya askari mamluki na vibaraka raia wa Saudi Arabia na Sudan.

Abdulqadir al Murtadha amesema kuwa Wasaudia walifanya jitihada za kuwa mpatanishi tu katika mazungumzo ya kubadilishana mateka lakini timu ya mazungumzo ya serikali ya Sana'a ilikubali mapatano ya kubadilishana mateka bila ya kuwepo Saudi Arabia katika meza ya mazungumzo. 

Al Murtadha amesema mateka wa Kiyamani wameteswa na kunyimwa matibabu katika korokoro za Saudia Arabia na wengi miongoni mwao wamepatwa na maradhi ya kuambukizwa.

Mateka wa Yemen baada ya kuwasili nyumbani

Amesema kuwa hadi ssa mateka 4,700 wa vita wameachiwa huru na ameziahidi familia za mateka waliosalia katika korokoro za wavamizi wa Yemen kwamba juhudi zinafanyika kuhakikisha kuwa mateka wote wanaachiwa huru.

Jumatano iliyopita operesheni kubwa zaidi ya kubadilisha matekani wa vita ilianza kutekelezwa baina ya Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen na serikali kibaraka ya rais wa zamani wa nchi hiyo, Abdrabbuh Mansur Hadi aliyetoroka nchi na kukimbilia Saudi Arabia.   

Tags