Oct 20, 2020 02:34 UTC
  • Sayyid Abdulmalik Badruddin al-Houthi
    Sayyid Abdulmalik Badruddin al-Houthi

Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema Marekani, Ufaransa na nchi zingine za Magharibi ndio waungaji mkono wa mwanzo kabisa wa makundi ya ukufurishaji huko Syria, Yemen na katika nchi zingine za Kiislamu kwa sababu zinawatumia wakufurishaji hao kuchafua jina la dini tukufu ya Uislamu.

Sayyid Abdulmalik Badruddin al-Houthi amebainisha kuwa, upotoshaji na upotokaji ni madhara mawili yaliyozusha mpasuko mkubwa katika safu za Waislamu na kusababisha matatizo makubwa.

Katibu Mkuu wa Ansarullah ameongeza kuwa, maadui wameutumia vibaya kwa maslahi yao upotoshaji unaofanywa ndani ya umma wa Kiislamu kwa ajili ya kuutusi Uislamu na Qur'ani tukufu.

Sayyid Abdulmalik al-Houthi ameeleza kuwa, katika ustaarabu wa Magharibi heshima ya jamii za wanadamu inakanyagwa, uhuru wa watu unahodhiwa, utajiri wao unaporwa na ardhi zao zinavamiwa na kukaliwa kwa mabavu, lakini pamoja na kufanya hayo ustaarabu huo unajinasibu kuwa mtetezi wa haki za binadamu.

Makundi ya wakufurishaji wanaotumiwa na Magharibi kuchafua sura ya Uislamu

Amebainisha pia kwamba, huko Magharibi ni marufuku kuwakosoa Wazayuni na kutilia shaka kwa namna yoyote mauaji ya Wayahudi ya Holocaust, lakini hukohuko Magharibi ni ruhusa mtu kuutusi na kuuvunjia heshima Uislamu na Mitume wa Mwenyezi Mungu.

Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema, migogoro iliyopo katika nchi za Kiislamu ni matokeo ya umamluki unaofanywa na baadhi kwa ajili ya maadui ya umma na matunda ya hujuma za Mkoloni Magharibi.../

Tags