Oct 24, 2020 04:43 UTC
  • Sudan yafuata mkumbo wa Imarati na Bahrain wa kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel

Viongozi wa Marekani, Sudan na utawala haramu wa Israel wametangaza katika taarifa yao pamoja juu ya kufikiwa makubaliano baina ya Tel-Aviv na Khartoum ya kuanzisha uhusiano wa kawaida baina yao.

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa, Rais wa Marekani Donad Trump, Luteni Jenerali Abdul-Fattah al-Burhan Kiongozi wa Baraza la Utawala la Sudan, Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdouk na Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala ghasibu wa Israel jana walizungumza kwa njia ya simu na kueleza kile walichokitaja kkuwa, hatua kubwa ya kihistoria iliyofikiwa na Sudan kuelekea demokrasia na kuunga mkono amani katika eneo.

Aidha taarifa hiyo ya pamoja imeeleza kwamba, makubaliano hayo yanalenga kuanzishwa uhusiano wa kiuchumi na kibiashara baina ya Sudan na utawala dhalimu wa Israel.

Hayo yanajiri katika ambayo katika majuma ya hivi karibuni, viongozi wa Sudan wamekuwa wakikanusha vikali taarifa za kuweko mpango wa nchi hiyo wa kuanzisha uhusiano na Israel.

Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Bahrain pamoja na Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Irael walipokuwa ikulu ya White House kutiliana saini makubaliano ya kutangaza uhusiano wa kawaida baina ya nchi zao na utawala ghasibu wa Israel.

 

Tayari shakhsia na vyama mbalimbali nchini Sudan vimelaani vikali habari hiyo ya kufikiwa makubaliano kati ya Sudan na Israel ya kuanzisha uhusiano baina yao.

Sudan inakuwa nchi ya tatu ya Kiarabu baada ya Imarati na Bahrain kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.

Tarehe 15 Septemba mwaka huu, Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Bahrain walitia saini makubaliano ya kutangaza uhusiano wa kawaida baina ya nchi zao na utawala ghasibu wa Israel.

Sherehe hizo zilizofanyika katika Ikulu ya Marekani, White House, zilihudhuriwa pia na Rais wa Marekani, Donald Trump na Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala dhalimu wa Israel.

Tags

Maoni