Oct 25, 2020 12:49 UTC
  • Harakati za mapambano Palestina zaapa kulipiza kisasi cha mauaji ya kijana Amer

Harakati za mapambano ya ukombozi wa Palestina zimetangaza kuwa zitajibu mauaji yaliyofaywa na askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya kijana aliyekuwa na umri wa miaka 18 wa Kipalestina katika Ukingo wa Magharibi kwa kuzidisha mapambano dhidi ya utawala huo.

Taarifa hiyo ya harakati za ukombozi za Palestina imetolewa baada ya askari wa utawala haramu wa Israel kumuua shahidi Amer Abedalrahim Snobar mapema leo Jumapili katika kijiji cha Yatma karibu na mji wa Turmus-Ayya, Kaskazini Mashariki mwa Ramallah.

Taarifa ya harakati ya Jihad Islamu ya Palestina imesema kuwa, kuuliwa shahidi kijana Amer Abedalrahim Snobar ni sehemu ya ugaidi wa kiserikali wa utawala haramu wa Israel, na imesisitiza udharura wa kuhuishwa aina zote za mapambano katia Ukingo wa Magharibi kwa ajili ya kukabiliana na uhalifu na ugaidi wa walowezi wa Kiyahudi na askari wa utawala wa Israel. 

Msemaji wa harakati ya Hamas, Hazem Qassem pia ametoa taarifa akitangaza kuwa, taifa la Palestina litalipiza kisasi cha mauaji ya Amer Snobar kwa kuzidisha mapambano na harakati ya Intifadha dhidi ya Wazayuni maghasibu.

Wakati huo huo Harakati ya Ahrar ya Palestina pia imetoa taarifa baada ya mauaji hayo ikisema: Mauaji ya Amer Snobar ni jinai nyingine inayosajiliwa katika faili chafu la utawala haramu wa Israel na kwamba Wapalestina watajibu mapigo kwa mapambano ya silaha na operesheni za kishujaa. 

Ahmed al-Bitawi, Mkurugenzi wa Kituo cha Matibabu cha Palestina (Palestine Medical Complex), amethibitishia mapema leo Jumapili kwamba Snobar ameaga dunia kutokana na majeraha aliyopata kutokana na shambulio la askari wa Israeli.

Kituo hicho kimesema kuwa, Snobar alijeruhiwa kwa kupigwa kwa vitako vya bunduki za wanajeshi wa Israeli. 

Tags

Maoni