Oct 25, 2020 16:44 UTC
  • Al Houthi: Kuna udharura wa kuwa na msimamo mmoja dhidi ya vitendo vya kuvunjiwa heshima Mtume Muhammad (saw)

Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Wananchi wa Yemen amesema kuna udharura wa kuwepo msimamo mmoja wa Kiislamu dhidi ya vitendo vya kuwavunjia heshima Mitume wa Mwenyezi Mungu.

Muhammad Ali al Houthi amelaani vikali kuvunjiwa heshima Mtume Muhammad (saw) nchini Ufaransa na amezitaka nchi za Kiislamu kuitisha kikao rasmi cha kulaani uhalifu huo.

Al Houthi pia amezitaka nchi za Waislamu kuushinikiza Umoja wa Mataifa ili upasishe sheria inayopiga marufuku vitendo vya kuvunjiwa heshima Mitume wa Mwenyezi Mungu. 

Kwa mara nyingine tena jarida la Kifaransa la Charlie Hebdo limeamua kwa makusudi kuwafanyia kejeli na istihzai Waislamu na dini yao tukufu kwa kuchapisha vibonzo vinavyomtusi na kumvunjia heshima Mtume Muhammad (SAW).

Jarida la Charlie Hebdo limeshapicha mara kadhaa katuni na vibonzo dhidi ya Uislamu na Mtume wake Muhammad (S.A.W) kwa kisingizio cha uhuru wa kujieleza, licha ya kukabiliwa na malalamiko makubwa ya Waislamu nchini Ufaransa na katika pembe mbalimbali za dunia. 

Waislamu Ufaransa wakipinga matamshi ya Macron

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa pia ameunga mkono vitendo hivyo viovu na kusisitiza kuwa, Ufaransa itaendelea kuchapisha vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw). 

Kufuatia matamshi hayo ya Macron, baadhi ya nchi za Kiislamu zimetoa wito wa kususiwa bidhaa za Ufaransa.  

Tags

Maoni