Oct 27, 2020 07:25 UTC
  • Mufti wa Oman: Waislamu waondoe mitaji yao katika sekta za uchumi za Ufaransa

Mufti wa Oman Sheikh Ahmed bin Hamad al-Khalili amewatolea mwito Waislamu wa kuondoa mitaji yao waliyowekeza kwenye vituo na sekta za uchumi za Ufaransa.

Sheikh Ahmed al-Khalili ameeleza katika taarifa kwamba, anaunga mkono kampeni ya kususia bidhaa za Ufaransa na akabainisha kuwa, kwa hatua yao ya kumvunjia heshima Bwana Mtume Muhammad SAW, viongozi wa Ufaransa wameonyesha kuwa hawajali wala hawathamini hisia za umma wa Kiislamu.

Mufti wa Oman amewataka Waislamu wachukue msimamo wa pamoja wa kuondoa mitaji yao katika vituo vya kiuchumi vya Ufaransa na kufanya juhudi za kuanzisha uchumi wao kimataifa ulio huru na wenye kujitegemea.

Hivi karibuni, jarida la Kifaransa la Charlie Hebdo lilichapisha tena vikatuni vya kumvunjia heshima Bwana Mtume Muhammad SAW. 

Matamshi ya Macron yamelaaniwa kila pembe ya Ulimwengu wa Kiislamu

Kufuatia malalamiko ya Waislamu wa Ufaransa, rais wa nchi hiyo Emmanuel Macron alitoa matamshi ya kifidhuli na yasiyoendana na adabu za kidiplomasia wala misingi ya demokrasia ya Magharibi aliposisitiza kuwa serikali yake itaendelea kuruhusu kuchapishwa vikatuni hivyo.

Matamshi na hatua hiyo ya Macron imelaaniwa vikali katika Ulimwengu wa Kiislamu, ambapo moja ya matokeo ya kusambaa wimbi la ghadhabu katika mataifa ya Kiislamu ni kuanzishwa kampeni ya kususia bidhaa za Ufaransa katika mataifa hayo.../

Tags