Oct 28, 2020 12:24 UTC
  • Wamarekani magaidi waendelea kuiba mafuta ya Syria

Duru mbalimbali za Syria zimetangaza habari ya kuendelea wizi wa mafuta ya nchi hiyo unaofanywa na wanajeshi magaidi wa Marekani.

Shirika rasmi la habari la Syria (SANA) leo Jumatano limetangaza habari ya kuendelea misafara ya malori ya mafuta ya wanajeshi magaidi wa Marekani kuiba mafuta ya Syria na kwenda nayo Iraq.

Habari ya karibuni kabisa kwa mujibu wa shirika hilo la habari ni ya malori 37 ya mafuta ambayo wanajeshi magaidi wa Marekani wameyaiba mashariki mwa Syria na kuyapeleka kimagendo nchini Iraq.

Mafuta ni miongoni mwa vyanzo vikuu vya pato la kigeni la serikali ya Syria. Kabla ya kuanza vita na magenge ya kigaidi mwaka 2011, Syria ilikuwa ikizalisha karibu mapipa laki 3 na 80 elfu kwa siku. Kwa sasa Marekani na makundi ya wanamgambo wa Kikurdi wanaofadhiliwa na nchi hiyo wanadhibiti maeneo yenye utajiri wa mafuta ya mashariki na kaskazini mashariki mwa Syria.

Lori la mafuta likipeperusha bendera ya Marekani nchini Syria

 

Miezi michache iliyopita, kampuni moja ya Marekani ilisaini mkataba na genge la waasi wa Kikurdi la Syrian Democratic Forces (SDF) kuhusiana na maeneo yenye utajiri wa mafuta yanayodhibitiwa na genge hilo.

Katika taarifa yake ya leo ya shirika la habari la SANA, magari kadhaa ya wanamgambo wa genge hilo SDF linalosaidiwa na wanajeshi magaidi wa Marekani yamesindikiza malori ya mafuta hayo ya wizi kwa msaada wa magari ya kijeshi ya Marekani.

Tags

Maoni