Nov 17, 2020 12:19 UTC
  • Uamuzi wa Trump wa kuitaja Ansarullah ya Yemen kuwa kundi la kigaidi

Kinyume na maoni ya mashirika ya kimataifa ya misaada ya kibinadamu, Rais Donald Trump wa Marekani ameazimia kuliweka kundi la Kiislamu la Ansarullah ya Yemen katika orodha ya nchi hiyo ya makundi ya kigaidi.

Wakizungumza jana Jumatatu na jarida la Foreign Policy wanadiplomasia kadhaa wa Marekani wamesema kuwa jambo hilo bila shaka litavuruga shughuli za mashirika ya kimataifa ya ufikishaji misaada ya kibinadamu katika pembe tofauti za nchi hiyo na hivyo kusimamisha ushirikiano ambao umekuwepo kati ya Umoja wa Mataifa na Ansarullah pamoja na serikali iliyojiuzulu ya nchi hiyo katika shughuli za ufikishaji misaada ya kibinadamu nchini Yemen.

Umoja wa Mataifa na mashirika hayo katika miezi ya hivi karibuni yamekuwa yakifanya juhudi kubwa za kuzuia kutekelezwa uamuzi wa Trump wa kuliweka kundi la Ansarullah katika makundi ya kigaidi lakini inavyoonekana ni kuwa huenda juhudi hizo zimefeli.

Abdul Malik al-Huthi, Kiongozi Mkuu wa Ansarullah

 

Makundi ambayo yamewekwa kwenye orodha ya ugaidi ya Marekani hayaruhusiwi kupewa msaada wala ushirikiano wowote na wanachama wake wanapigwa marufuku kusafiri nchini Marerekani na pia akaunti zao za benki katika nchi za nje kufungwa.

Umuzi ho unakaribia kuchukuliwa katika hali ambayo Marekani yenyewe imekuwa ikunga mkono uvamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya Yemen tokea Machi 2015, uvamizi ambao hadi sasa umepelekea zaidi ya Wayemen 16,000 kupoteza maisha, makumi ya maelefu kujeruhiwa na mamilioni kulazimika kuishi kama wakimbizi.

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wameutaja mgogoro wa Yemen kuwa mgogoro mbaya zaidi wa kibidamu duniani.

Tags