Nov 20, 2020 07:47 UTC
  • Umoja wa Mataifa wapasisha azimio la haki ya Wapalestina ya kujiainisha hatima yao

Umoja wa Mataifa umepasisha azimio linalotilia mkazo haki walionayo Wapalestina ya kujiainishia hatima na mustakabali wao.

Azimio hilo limepasishwa kwa wingi wa kura 163 za ndio, 5 za hapana na wawakilishi wa nchi 10 wakijizuia kupiga kura.

Azimio hilo lililopasishwa katika kamati ya tatu ya Kamisheni ya Masuala ya Kijamii, Kiutu na Kiutamaduni ya Umoja wa Mataifa kwa wingi wa kura linasisitiza kuwa, wananchi wa Palestina wana haki ya kisheria ya kujiainishia mustakabali wao kama kuwa na dola lao huru.

Aidha azimio hilo linayataka mataifa yote pamoja na asasi na mashirika yenye mfungamano na Umoja wa Mataifa kuliunga mkono taifa la Palestina na kushirikiana na wananchi hao kwa ajili ya kufikia lengo lao la kujiainishia hatima na mustakabali wao kwa haraka na katika kipindi cha muda mfupi kadiri inavyowezekana.

Bendera ya Palestina

 

Sehemu nyingine ya azimio hilo la Umoja wa Mataifa inasisitiza kuhitimishwa haraka iwezekanavyo ukaliaji mabavu wa ardhi za Palestina unaofanyawa na utawala haramu wa Israel.

Hata hivyo maazimio ya Umoja wa Mataifa yamekuwa hayatekelezwi na utawala haramu wa Israel.

Wajuzi wa mambo wanasema kuwa, uungaji mkono wa Marekani kwa utawala haramu wa Israel umekuwa ukiupa kiburi utawala huo ghasibu na kuupandisha kichwa cha kuendelea na siasa zake za kidhalimu dhidi ya Wapalestina bila ya kujali hasira za walimwengu.

Tags