Nov 21, 2020 12:01 UTC
  • Afisa wa Yemen; Saudi Arabia imekusudia kuukabidhi mkoa wa Abyan kwa magaidi wa al Qaida

Gavana wa mkoa wa Abyan huko Yemen amesema kuwa Saudi Arabia inafanya kila inaloweza kuukabidhi mkoa wa Abyan kwa mtandao wa kigaidi wa al Qaida.

Saleh al Junaidi leo Jumamosi ameeleza kuwa, Saudi Arabia kwa kiasi kikubwa inafanya juhudi ili kuugeuza mkoa huo kuwa sehemu ya mapigano baina ya makundi yenye mfungamano nayo. Amesema Saudia inafanya hivyo lengo likiwa ni kuwalazimisha kuhama kwa umati kwenye makazi yao mamia ya familia zinazoishi katika mji wa Zinjibar na karibu na nukta za mapigano huko Sheikh Salem, al Tariya na Wada Salam.  

Gavana wa mkoa wa Abyan amezitaja nchi vamizi na makundi ya wanamgambo yenye mfungamano na nchi hizo kuwa chanzo cha maafa na taathira mbaya za mapigano yanayojii huko Abyan na kuwataka mashekhe wa makabila mbalimbali na shakhsia wenye taathira katika jamii kusambaratisha njama hiyo ya adui mvamizi ambayo imekuwa ikitekelezwa kwa zaidi ya miaka miwili sasa. 

Al Junaidi amesisitiza kuwa, Saudi Arabia inafanya kila inaloweza ili kuyaunga mkono makundi ya kitakfiri na kuyakingia kifua katika miji kadhaa ya mkoa wa Abyan; na kwamba ushahidi wote wa kuaminika unaonyesha kuwa magaidi wa al Qaida wapo kaika mikoa ya kusini mwa Yemen na misaada ya kifedha ya Saudia kwa mamluki wa kitakfiri katika mkoa wa Abyan ipo wazi. 

Magaidi wa al Qaida katika mkoa wa Abyan, Yemen 

Tags