Nov 22, 2020 06:29 UTC
  • Saudia yakiri tena hadharani kuwa inauunga mkono utawala wa Kizayuni

Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia amekiri tena hadharani kwamba nchi yake inaunga mkono kuwa na uhusiano kamili wa kawaida na utawala dhalimu wa Israel.

Shirika la habari la ISNA limeripoti habari hiyo leo Jumapili na kumnukuu waziri wa mambo ya nje wa Saudia, Faisal bin Farhan Aal Saud akisema hayo pambizoni mwa mkutano wa G20 mjini Riyadh na kuongeza kuwa, nchi yake daima imekuwa muungaji mkono wa uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa ajili ya kufikia amani ya kudumu.

Tangu zamani ukoo wa Aal Saud una uhusiano mzuri na Wazayuni maghasibu

 

Kabla ya hapo pia, Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia alikuwa ametangaza kwamba nchi yake inaunga mkono uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Kizayuni licha ya kwamba utawala huo pandikizi unafanya jinai kubwa dhidi ya Wapalestina.

Amma kuhusiana na matokeo ya uchaguzi wa Marekani, waziri huyo wa mambo ya nje wa Saudi Arabia amesema, ana yakini kwamba serikali ijayo ya Marekani itafuata siasa zile zile za huko nyuma za nchi hiyo kuhusu eneo hili na kwamba hakutokuwepo mabadiliko yoyote katika uhusiano wa Riyadh na Washington.

Matamshi hayo ya waziri wa mambo ya nje wa Saudia yametolewa katika hali ambayo, rais mteule wa Marekani, Joe Biden alidai kabla ya uchaguzi wa rais huko Marekani kwamba iwapo atashinda uchaguzi huo, ataangalia upya uhusiano wa Washington na Riyadh.

Tags