Nov 23, 2020 13:00 UTC
  • Unicef  kugawa dozi bilioni 2 za  chanjo ya corona  kwa nchi maskini duniani

Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangza kuwa unataraji kugawa dozi bilioni mbili za chanjo ya maradhi ya Covid-19 kwa nchi maskini duniani.

Unicef leo imetangaza kuwa shirika hilo mwaka ujao wa 2021 limepanga kugawa kwa nchi maskini na zinazoendelea duniani chanjo za corona chini ya mkakati wa uwezeshaji upatikanaji wa chanjo hiyo (COVAX) katika fremu ya mpango wa kimataifa wa ugawaji chanjo ya kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19. Shirika la Unicef linashirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) katika zoezi hilo.  

Yemen na maambukizi ya kirusi cha corona 

Mfuko wa Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa aidha umesisitiza kuwa, hivi sasa unashirikiana na mashirika 350 ya ndege na usafiri wa meli ili kusafirisha chanjo za kujikinga na kirusi cha corona na sirinji bilioni moja katika nchi maskini kama Burundi, Afghanistan na Yemen. 

Takwimu zinaonyesha kuwa, hadi sasa watu milioni 59 elfu 32 na 743 duniani wamepatwa na kurusi cha corona huku watu wengine milioni 1, laki tatu na 94,389 wakiaga dunia mwa maradhi hayo.

Tags