Nov 25, 2020 08:09 UTC
  • Ansarullah: Jibu lijalo la Wayemen kwa wavamizi litakuwa kali zaidi

Harakati ya Ansarullah ya Yemen imeonya kuwa jibu lijalo litakalotolewa kwa Wasaudia wavamizi litakuwa kali zaidi na pia kubwa zaidi kuliko la kiwanda cha kusafisha mafuta cha Aramco.

Ali al Qahum, mjumbe mwandamizi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen ameieleza kanali ya televisheni ya Al Mayadeen kwamba hali ya kutapatapa uliyonayo utawala wa Aal Saud kufuatia shambulio la makombora lililofanywa na vikosi vya ulinzi vya Yemen dhidi ya kiwanda cha kusafisha mafuta cha Aramco kilichoko mjini Jeddah inadhihirisha kuzidi kuongezeka nguvu na uwezo wa vikosi vya ulinzi vya Yemen.

Usiku wa kuamkia jana, msemaji wa vikosi vya ulinzi vya Yemen Yahya Saree alitangaza kuwa, kikosi cha makombora cha jeshi la Yemen kimeshambulia kwa kombora linaloongozwa kulenga shabaha maalumu la Quds 2 kituo cha ugavi cha vinu vya mafuta vya Aramco nchini Saudia.

Shambulio la vikosi vya ulinzi vya Yemen kwa kiwanda cha kusafishia mafuta cha Aramco, Saudia

Wakati huohuo, katika kile kinachoonekana kama ishara ya kubabaika na kutapatapa kutokana na jibu la shambulio la makombora la vikosi vya ulinzi vya Yemen dhidi ya taasisi nyeti na hasasi za Saudi Arabia, utawala wa Aal Saud umeishtaki harakati ya Ansarullah ya Yemen kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Saudia imelitaka Baraza la Usalama lisimamishe kile ilichokiita, tishio kwa usalama wa nishati duniani, kwa mchakato wa kisiasa hasa wa nchini Yemen na kwa amani ya eneo.../

Tags