Dec 01, 2020 07:35 UTC
  • Wamorocco wachoma moto bendera ya Israel katika kuonyesha mshikamano wao na Palestina

Wananchi wa Morocco wamechoma bendera ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kushikana na Taifa la Palestina.

Wananchi wa Morocco walichoma moto bendera ya utawala wa Kizayuni mkabala na jengo la bunge la nchi hiyo huko Rabat katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kushikamana na Palestina. 

Maandamano hayo yamehudhuriwa na shakhsia wa kisiasa na wa makundi ya kiraia kutoka matabaka mbalimbali kufuatia mwaliko wa taasisi 54 za nchini humo. Washiriki katika maadhimisho hayo wamelaani jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Palestina na kupiga nara wakipinga mwenendo wa kuanzisha uhusiano wa kawaida kati ya nchi za Kiarabu na utawala wa Kizayuni wa Israel.  

Mfalme Mohammed wa Sita wa Morocco ametuma ujumbe kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kushikamana na Taifa la Palestina na kueleza kuwa, suala la Palestina ni kadhia muhimu yenye lengo la kuyapatia ufumbuzi wa kudumu matatizo mbalimbali katika eneo. 

Mlame Mohammed wa Sita wa Morocco 

Rais Donald Trump wa Marekani mwishoni mwa uongozi wake amefanya jitihada ili kufanikisha kuanzishwa uhusiano wa kawaida  kati ya baadhi ya nchi za Kiarabu na utawala wa Kizayuni. Miongoni mwa nchi hizo za Kiarabu zilizoanzisha uhusiano wa kawaida na Israel ni Imarati, Bahrain na Sudan. Hatua ya nchi hizo ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Kizayuni imepingwa na kukosolewa vikali katika Ulimwengu wa Kislamu.

Tags