Jan 03, 2021 13:29 UTC
  • Watalii kutoka Israel waingiza kimagendo madawa ya kulevya nchini Imarati

Baadhi ya vyombo vya habari vya Kiebrania vimetangaza kuwa, watalii kutoka Israel wanaoelekea Umoja wa Falme za Kiarabu wanaingiza kimagendo madawa ya kulevya katika nchi hiyo ya Kiarabu.

Kanali ya 12 ya televisheni ya utawala wa Kizayuni wa Israel imetangaza kuwa, watalii wapatao elfu nane wameelekea Dubai kusherehekea mwaka mpya wa 2021 wakiwa wameficha kwenye makatuni ya sigara na soksi zao makumi ya tani za bangi na kasumba walizoingia nazo nchini Imarati.

Hapo kabla, kanali hiyo ya televisheni ya Kizayuni iliripoti kuwa, watalii kutoka Israel wameugeuza mji wa Dubai kuwa kitovu cha ufisadi na ufuska.

Gazeti la Kizayuni la Yediot Ahronot liliandika katika toleo lake la siku ya Jumanne iliyopita kuwa, watalii kutoka Israel wanaiba kila wanachoweza kukibeba katika hoteli wanazofikia nchini Imarati.

Itakumbukwa kuwa Imarati ilikuwa nchi ya kwanza ya Kiarabu ya eneo la Ghuba ya Uajemi ambayo mnamo tarehe 13 Agosti mwaka jana, na kwa upatanishi wa serikali ya rais Donald Trump wa Marekani, ilitangaza rasmi kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.../

Tags