Jan 05, 2021 14:19 UTC
  • Athari mbaya za silaha za Marekani nchini Iraq
    Athari mbaya za silaha za Marekani nchini Iraq

Mshauri wa masuala ya kisheria wa Bunge la Iraq amefungua mashtaka dhidi ya Marekani katika mahakkama ya Sweden kwa tuhuma za kukiuka mamlaka ya kujitawala ya Iraq na kutumia silaha zenye uranium dhidi ya nchi hiyo.

Hatef al Rikabi amesema kuwa, amewasilisha mashtaka hayo katika mahakkama ya Sweden akitaka Iraq ilipwe fidia kutokana na uharibivu uliosababishwa na silaha, mabomu na makombora yenye mada ya uranium ya Marekani katika kipindi chote cha miongo kadhaa iliyopita.

Al Rikabi amesema kuwa, mbali na mashambulizi ya Marekani dhidi ya miji na maeneo mbalimbali ya Iraq, utawala wa Kizayuni wa Israel pia ulishambulia kinu cha nyuklia cha Tammuz mwaka 1981 nchini Iraq, mashambulizi ambayo yamesababisha maafa makubwa kwa mamia ya maelfu ya Wairaqi kwa sababu ya kuathiriwa na miali ya uranium na kwamba hadi sasa ardhi ya Iraq unaendelea kuuathiriwa na miali hiyo.

Amesema kuwa msiba mkubwa zaidi ni kwamba, katika miaka yote iliyopita utawala wa Iraq haukusafisha sumu zilizosababisha na mashambulizi hayo na wala haukuitaka jamii ya kimataifa iilazimishe Marekani kulipa fidia kutokana na uharibifu huo. 

Maelfu ya Wairaqi wameathiriwa na silaha zenye sumu za Marekani

Hivi karibuni taasisi inayojulikana kama Mtandao Mpana wa Upashaji Habari wenye makao yake mjini na Nairobi, Kenya iligundua nyaraka za siri kuhusu ukiukaji wa sheria unaofanywa na Marekani ambazo zinafichua kuwa, jeshi la Marekani nchini Iraq limetumia silaha zenye mada ya urani iliyohafifishwa, kwa uchache mara 116, kulenga vituo vya jeshi, makazi na magari madogo na makubwa.

Tags