Jan 08, 2021 02:42 UTC
  • Mshauri wa Rais wa Syria: Qassem Suleimani alikuwa kamanda wa nyoyo na mpamabanaji wa njia ya ukombozi

Mshauri maalumu wa Rais Bashar al Assad wa Syria amesema, shahidi Qassem Suleimani alikuwa mpigania uadilifu kwa ajili ya wanadamu na mpambanaji wa njia ya ukombozi.

Buothaina Shaaban, ambaye kwa niaba ya rais wa Syria alishiriki katika maadhimisho ya mwaka wa kwanza wa kumbukumbu ya kuuawa shahidi kamanda Qassem Suleimani, yaliyofanyika jana Alkhamisi mjini Damascus, amesema katika hotuba aliyotoa katika maadhimisho hayo kwamba, kwa ajili ya kuthibitisha kiwango cha taathira na adhama ya shahidi Suleimani, inatosha kujua kwamba yeye hakufanya harakati za kutaka atambulike wakati wa uhai wake, ilhali katika kipindi cha miaka yote hii na kwa muda wote alikuwa mfano hai wa muqawama dhidi ya ukoloni kutokana na alivyopambana kuilinda Iran, Syria, Lebanon, Iraq na Yemen.

Bouthaina Shaaban

Bi Bouthaina Shaaban amesema, msingi uliowekwa na mashahidi Qassem Suleimani na Abu Mahdi al Muhandis ni fikra ya kistratejia na mfano wa kuigwa na vizazi vijavyo; na akaongeza kuwa, hatua walizochukua mashahidi hao wawili wa muqawama ilizishughulisha na kuzitia tafrani fikra za Wazayuni; na hatua ya kigaidi iliyochukuliwa na maadui dhidi ya mashahidi hao ililenga kufuta marejeo na mwega mkuu wa makamanda wa ushindi katika kukabiliana na uvamizi na ukaliaji ardhi kwa mabavu.

Luteni Jenerali Qassem Suleimani, ambaye mnamo usiku wa kuamkia tarehe 3 Januari 2020 alielekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo, aliuawa shahidi alfajiri ya kuamkia siku hiyo yeye na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Mkuu wa jeshi la kujitolea la wananchi wa Iraq Al Hashdu-Sha'abi pamoja na wanamuqawama wengine wanane, katika shambulio la anga lililofanywa na jeshi la kigaidi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad.../

 

 

Tags