Jan 08, 2021 02:43 UTC
  • Makombora yenye shabaha kali ya Lebanon, Syria, Yemen na Iran ndilo tishio kubwa zaidi kwa Israel 2021

Kituo cha tafiti za usalama wa ndani cha utawala haramu wa Kizayuni wa Israel kimetangaza kuwa tishio kubwa zaidi kwa utawala huo katika mwaka huu wa 2021 ni makombora yenye shabaha kali ya Lebanon, Syria, Yemen na Iran.

Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti kiliofanya, kituo hicho cha utawala haramu wa Israel kimesisitiza kuwa, kuanzia mwaka 2020 na kwa sababu ya kile ilichokitaja kuwa ni kujitoa Iran kwenye mapatano ya nyuklia na kupiga hatua kubwa tafiti za Tehran katika sekta ya makombora, mabadiliko yameanza katika mlingano wa hali ya usalama wa ndani na kufifia kwa nguvu za jeshi la Israel.

Kituo hicho za Kizayuni kimesisitiza pia kwamba, changamoto nyingine itakayoukabili utawala haramu wa Israel katika mwaka 2021 ni kuruhusiwa baadhi ya nchi za Kiarabu kununua silaha kwa Marekani kupitia "makubaliano ya mapatano" na uhusiano wa utawala wa Kizayuni na serikali ya rais mteule wa nchi hiyo Joe Biden.

Ripoti ya kituo cha tafiti za usalama wa ndani cha utawala haramu wa Kizayuni wa Israel imeashiria pia kwamba katika mwaka 2021, itapasa utawala wa Tel Aviv uchukue hatua ya kuzijumuisha Misri, Jordan na Mamlaka ya Ndani ya Palestina katika mashirikiano ya pamoja ya kikanda na vilevile kuzuia kuongezeka nguvu za kijeshi za harakati ya Hamas au hata shambulio la kijeshi la harakati hiyo dhidi ya utawala huo haramu.../

Tags