Jan 08, 2021 02:44 UTC
  • Mahakama ya Iraq yaamuru Trump akamatwe kwa mauaji ya makamanda wa muqawama

Mahakama ya Ar-Rasaafah nchini Iraq inayofuatilia kesi ya mauaji ya makamanda wa muqawama Luteni Jenerali Qassem Suleimani na Abu Mahdi al-Muhandis imetoa waranti wa kukamatwa rais wa Marekani Donald Trump.

Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Iraq WAA, hakimu maalum wa mahakama ya uchunguzi ya Ar-Rasaafah ametoa taarifa maalum na kutangaza kwamba, baada ya kukamilika mchakato wa kukusanya madai ya walalamikaji binafsi wa faili la kesi hiyo na pia uchunguzi wa awali, ametoa waranti wa kutiwa nguvuni Trump.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uchunguzi utaendelea kufanywa kuwatambua wahusika wengine walioshiriki katika jinai ya mauaji hayo, wawe ni Wairaqi au raia wasio Wairaqi.

Majemadari wa muqawama

Luteni Jenerali Qassem Suleimani, ambaye mnamo usiku wa kuamkia tarehe 3 Januari 2020 alielekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo, aliuawa shahidi yeye na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Mkuu wa jeshi la kujitolea la wananchi wa Iraq Al Hashdu-Sha'abi pamoja na wanamuqawama wengine wanane katika shambulio la anga lililofanywa na jeshi la kigaidi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad.

Kufuatia kuuawa shahidi makamanda hao wa muqawama, bunge la Iraq lilipitisha mpango unaowataka askari wa jeshi la kigaidi la Marekani waondoke nchini humo.../

Tags