Jan 09, 2021 12:54 UTC
  • Hizbullah: Kumwekea vikwazo Mkuu wa Al-Hashdu-Sha'abi ni mwendelezo wa jinai za Marekani

Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imesema, hatua ya Marekani ya kumwekea vikwazo Mkuu wa Jeshi la kujitolea la wananchi wa Iraq la Al-Hashdu-Sha'abi ni "jinai".

Ofisi ya udhibiti wa mali za kigeni ya wizara ya fedha ya Marekani ilitangaza jana usiku kuwa, jina la Falih al-Fayyaz, Mkuu wa Al-Hashdu-Sha'abi ya Iraq limewekwa kwenye orodha ya vikwazo ya Washington.

Katika jibu ililotoa kwa hatua hiyo ya Marekani ya kumwekea vikwazo Falih al-Fayyaz, Harakati ya Hizbullah ya Lebanon leo imetoa taarifa na kueleza kwamba, vikwazo hivyo ni nyongeza ya mlolongo wa jinai zinazoendelea kufanywa na Marekani dhidi ya Iraq na watu wake.

Katika taarifa yake hiyo, Hizbullah imesema, sababu kuu ya Salih al-Fayyaz kuwekewa vikwazo na Marekani ni msimamo wake thabiti kuhusiana na uvamizi wa Marekani na kutokubali kuhalalisha uwepo wa wavamizi hao katika ardhi ya Iraq na vilevile nafasi ya Al-Hashdu-Sha'abi katika kupambana na magaidi wa DAESH (ISIS).

Kitambo si kirefu nyuma, Falih al-Fayyaz, Mkuu wa Al-Hashdu-Sha'abi ya Iraq alitoa indhari kuhusu njama zinazofanywa kwa lengo la kuchafua jina la jeshi hilo la kujitolea la wananchi wa Iraq.../

Tags