Jan 18, 2021 11:56 UTC
  • Mbali na mafuta, Marekani sasa inaiba mazao ya mashamba ya Wasyria

Sambamba na kuendelea wizi wa mafuta ya Syria unaofanywa na wanajeshi magaidi wa Marekani, askari hao vamizi sasa wameanza kupora mazao ya mashamba ya wananchi wa nchi hiyo ya Kiarabu.

Duru za habari zimeliambia shirika rasmi la habari la Syria (SANA) kuwa, msafara wa magari kadhaa ya wanajeshi wa Marekani yaliyobeba bidhaa hizo za kilimo ulionekana jana Jumapili ukielekea kaskazini mwa Iraq kwa kutumia kivuko haramu cha al-Walid katika mkoa wa Hasaka, kaskazini mashariki mwa Syria.

Habari zaidi zinasema kuwa, wanajeshi wa Marekani wameiba mazao hayo kutoka katika mashamba ya wakulima wa Syria katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na askari hao vamizi katika eneo la al-Jazeera.

Inaarifiwa kuwa, malori yasiyopungua 20 ya jeshi la Marekani yamepeleka nchini Iraq nafaka zilizoibwa kutoka kwenye mabohari ya kuhifadhi bidhaa za kilimo viungani mwa mkoa wa Hasaka, kaskazini mashariki mwa Syria.

Kwa muda mrefu sasa, malori ya mafuta ya wanajeshi magaidi wa Marekani yamekuwa yakiiba mafuta ya Syria na kuyapeleka Iraq.

Malori ya US yakisafirisha mafuta ya wizi kwenda Iraq

Mafuta ni miongoni mwa vyanzo vikuu vya pato la kigeni la serikali ya Syria. Kabla ya kuanza vita na magenge ya kigaidi mwaka 2011, Syria ilikuwa ikizalisha karibu mapipa laki 3 na 80 ya mafuta elfu kwa siku.

Kwa sasa Marekani na makundi ya wanamgambo wa Kikurdi wanaofadhiliwa na nchi hiyo ya kibeberu wanadhibiti maeneo yenye utajiri wa mafuta ya mashariki na kaskazini mashariki mwa Syria.

Tags