Jan 21, 2021 11:43 UTC
  • Hamas: Trump alikuwa mshirika wa hujuma za utawala wa Kizayuni dhidi ya Palestina

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesisitiza kuwa Donald Trump alikuwa mshirika wa moja kwa moja wa utawala wa Kizayuni katika kuwakandamiza wananchi wa Palestina.

Gazeti la al Quds al Arabi leo limeripoti kuwa, Fauz Barhum Msemaji wa Harakati ya Muqawama ya Palestina (Hamas) ameeleza kuwa: Rais Mpya wa Marekani Joe Biden anapasa kubadili mwenendo wa siasa mbovu na zisizo za kiuadilifu za viongozi wa Marekani mkabala na wananchi wa Palestina na kuanzisha msingi wa usalama na uthabiti katika eneo.  

Barhum amemtaka Biden kufuta maamuzi yote yanayohusiana na juhudi za kusambaratisha malengo ya Palestina khususan maamuzi yanayohusiana na Baitul Muqaddas na wakimbizi wa Palestina; na kuheshimu irada ya wananchi wa Palestina na machaguo yao ya Kidemokrasia.  

Makundi ya Kipalestina pia jana Jumatano yalilaani matamshi ya Antony Blinken Waziri Mambo ya Nje aliyependekezwa na Biden kwamba Marekani ingali inaitambua Quds inayokaliwa kwa mabavu kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni na haiko tayari kuurejesha ubalozi wake huko Tel Aviv.  

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani aliyependekezwa na Joe Biden 

Uongozi wa miaka minne wa Rais Donald Trump ulimalizika jana Jumatano; na Joe Biden ameanza kazi kama Rais mpya wa Marekani.  

 

Tags