Jan 25, 2021 07:50 UTC
  • Marekani, Saudia na Israel zinachochea hujuma za kigaidi Iraq

Harakati ya Kata'ib Hizbullah ya Iraq imesema hujuma za kigaidi ambazo zimetekelezwa na kundi la kigaidi la ISIS nchini humo zinachochewa na muungano wa Marekani, Saudi Arabia na Israel.

Abdul Ali al-Asgari, Mkuu wa Masuala ya Usalama katika Katai'b Hizbullah ametoa kauli hiyo katika ujumbe wa Twitter siku ya Jumapili. Katika ujumbe huo ameandika: "Wanaotekeleza mauaji nchini Iraq ni Marekani, Saudi Arabia na Israel na hivyo ulipizaji kisasi unapaswa kulenga chanzo au msingi na si matawi."

Matamshi hayo yanakuja baada ya mashambulizi pacha yaliyotekelezwa na kundi la kigaidi la ISIS katika mtaa wenye shughuli nyingi mjini Baghdad siku ya Alhamisi ambapo raia 32 walipoteza maisha na wengine 110 kujeruhiwa. Aidha magaidi wa ISIS siku ya Jumapili waliwashambulia na kuwaua maafisa 11 wa Jeshi la Kujitolea la Wananchi wa Iraq (PMU) maarufu kama Hashd al-Shaabi katika mkoa wa Salahuddin. Wapiganaji wa Hashd al-Shaabi wamepata umaarufu nchini Iraq kutokana na mafanikio yao katika oparesheni za kuangamiza magaidi wa ISIS.

Magaidi wa ISIS

Magaidi wa ISIS au Daesh wanafuata itikadi ya ukufurishaji ya pote la Uwahhabi ambalo linatawala Saudi Arabia. Taarifa za kiintelijensia zinasema magaidi wa ISIS wamekuwa wakipokea misaada ya siri kutoka Marekani, Israel na Saudi Arabia katika kampeni yao ya uharibufu na mauaji huko Iraq na Syria tokea mwaka 2014.

 

Tags