Jan 25, 2021 23:39 UTC
  • Abdul-Salaam al-Wajih: Watawala wa Saudia, Imarati na Bahrain ni mamluki wa mipango ya kikoloni ya Marekani na Israel

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maulamaa wa Yemen amesema kuwa, watawala wa Saudi Arabia, Imarati na Bahrain ni watekelezaji wa mipango ya kikoloni ya Marekani na utawala haramu wa Israel.

Abdul-Salaam al-Wajih amesisitiza kuwa, vita ilivyotwishwa nchi ya Yemen ni vita vya Uzayuni-Marekani ambavyo vinaulenga Umma wote wa Kiislamu.

Kiongozi huyo wa Jumuiya ya Maulamaa wa Kiislamu nchini Yemen amebainisha kuwa, lengo hasa la vita dhidi ya Yemen ni kuugawa Ulimwengu wa Kislamu nan chi za Kiarabu.

Kadhalika Abdul-Salaam al-Wajih amesema kuwa, lengo jingine la viita dhidi ya Yemen ni kuusaidia utawala dhalimu wa Israel na kuanzisha kambi za kijeshi za utawala huo ghasibu katika visiwa na bandari za Yemen.

Mfalme wa Saudia Salman bin Abdul-Aziz akimvisha medali Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump

 

Katibu Mkuu huyo wa Jumuiya ya Maulamaa wa Yemern azitaja koo za Aal Saud, Al-Nahyan na Aal Khalifa kuwa ni mamluki watuumwa ambao wako kwa ajili ya kutekeleza mipango ya kikoloni ya Marekani na Israel.

Hata hivyo, amewataka viongozi wa mataifa hayo aliyoyataja kuwa wasaliti kwamba, mipango yao hiyo michafu itafeli na kushindwa.

Vilevile Katibu Mkuu huyo wa Jumuiya ya Maulamaa wa Kiislamu wa Yemern amesema kuwa, katika historia yake ndefu Yemen ilikuwa, imekuwa na itaendelea kuwa makaburi ya wavamizi, na kuongeza kwamba, Inshallah, Haram Mbili za Makka na Madina zitakuwa katika mkondo wa kukombolewa Quds Tukufu.