Jan 31, 2021 07:34 UTC
  • Al Kadhimi asisitiza kulipiza kisasi kwa wahusika wa milipuko ya Baghdad

Waziri Mkuu wa Iraq amesisitiza kuwa, wale wote walioihusika katika kuwaua raia wasio na hatia katika milipuko ya karibuni katika maidani ya al Tayaran huko Baghdad mji mkuu wa nchi hiyo watalipizwa kisasi.

Mustafa al Kadhimi Waziri Mkuu wa Iraq amezitembelea familia za watu waliopoteza maisha katika milipuko ya kigaidi huko Baghdad na kueleza kuwa, vyombo vyote ya usalama, intelijinsia na kijeshi vya Iraq usiku na mchana vinamsaka Abu Yasir al Issawi gavana wa Daesh huko Iraq na mamluki na wapangaji wengine wa jinai hiyo iliyotekelezwa katika maidani ya al Tayaran. 

Al Kadhimi ameongeza kuwa, matabaka yote ya wananchi na makundi ya Iraq yanapasa kushiriki katika kuunda serikali imara, iliyo huru na yenye nguvu.  

Alhamisi tarehe 21 mwezi Januari mwaka huu milipuko miwili mikubwa ya kigaidi ilitokea katika eneo la al Bab Shaqi huko Baghdad na kuua watu 32 na kujeruhi wengine 110. Hiyo ni kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya ya Iraq. Vikosi vya usalama vya nchi hiyo vimewatia mbaroni watu 60 wakiwemo vinara kadhaa wa ngazi ya juu wa kundi la kigaidi la Daesh kufuatia milipuko hiyo.  

Milipuko pacha katika maidani ya al Tayaran huko Baghdad, Iraq 

 

Tags