Feb 23, 2021 02:44 UTC
  • Umoja wa Maulamaa wa Kiislamu: Sehemu kubwa ya Madaesh wa kujiripua wameingia Iraq kutokea Syria

Mkuu wa Umoja wa Maulamaa wa Kiislamu katika mkoa wa Diyala nchini Iraq amesema kuwa, sehemu kubwa ya magaidi wa Daesh (ISIS) wa kujiripua kwa mabomu wameingia nchini Iraq wakitokea Syria.

Sheikh Jabar al Maamuri alisema hayo jana Jumatatu katika mahojiano na mtandao wa habari wa al Maaluma na kuongeza kuwa, miaka mitatu iliyopita Umoja wa Maulamaa wa Kiislamu ulionya kuhusu hatari ya kuweko maelfu ya magaidi wa Daesh katika maeneo tofauti ya Syria hususan kwenye mpaka wa nchi hiyo na Iraq.

Amesema, kutokana na Marekani kukwamisha juhudi zote za kimataifa za kuangamizwa mabaki ya genge la kigaidi ya Daesh, kazi ya kuliangamiza kikamilifu genge hilo inachukua muda mrefu. Amesema, Marekani inawatumia magaidi wa Daesh kama mabomu ya saa na kwamba sehemu kubwa ya magaidi waliouawa kabla ya kufanya mashambulio ya kujiripua kwa mabomu huko Diyala, Salahuddin, al Anbar na pembeni mwa Baghdad wameingia Iraq wakitokea Syria na wengi wao wamepewa mafunzo ya kigaidi ndani ya Syria.

Sayyid Jabar al Maamuri

 

Mkuu wa Umoja wa Maulamaa wa Kiislamu amesisitiza kuwa, sasa hivi Iraq inakabiliwa na njama mpya ya kuhatarisha usalama, kuchochea machafuko na kuvuruga utulivu katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Amesema, usalama wa Iraq utapatikana kwa kuangamizwa kikamilifu magaidi wa ISIS nchini Syria au kwa uchache kuimarishwa usalama katika mipaka ya nchi hizo mbili na kutoruhusiwa gaidi yeyote yule kupenya na kuingia nchini Iraq.

Sasa hivi kuna maelfu ya magaidi wa Daesh wanaolindwa na wanajeshi vamizi na magaidi wa Marekani nchini Syria licha ya Washington kudai kiuongo kuwa inapambana na magaidi hao wa ISIS.

Tags