Feb 25, 2021 07:37 UTC
  • Maulamaa wa Muqawama: Ushindi katika kuikomboa Quds hauna shaka

Mkuu wa Jumuiya ya Maulamaa wa Muqawama amesisitiza kuwa, kwa kudumisha Waislamu umoja na mshikamano, mapamban ya kuuikomboa Baytul- Muqaddas yatapa ushindi.

Sheikh Mahir Hamoud amesisitiza kuwa: Tunawaambia wale wote wanaodai kuwa ni Waislamu na wanashikamana na Uislamu na ambao wamenyanyua juu bendera ya kupigania uadilifu kwamba, bila ya Palestina na bila ya kuyapa umuhimu malengo matukufu ya Palestina kama kukombolewa Quds, basi nara zenu zina mapungufu na hazijakamilka.

Mkuu huyo wa Jumuiya ya Maulamaa wa Muqawama amesema kuwa, Waislamu wote wanapaswa kuungana na kuwa kitu kimoja katika njia ya kukomboa Palestina na wajiepushe na taasubi na chuki ambazo zinawaweka mbali na njia hii.

Sheikh Mahir Hamoud, Mkuu wa Jumuiya ya Maulamaa wa Muqawama

 

Hayo yanajiri katika hali ambayo, hivi karibuni Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) ililaani njama za utawala haramu wa Israel dhidi ya Baitul-Muqaddas na kusisitiza kuwa, siasa za utawala wa Kizayuni wa Israel za kuiyahudisha Quds zimeshindwa na kugonga mwamba na kwamba, Quds utabakia kuwa mji mkuu wa milele wa Palestina.

Sambamba na hayo, Wazayuni wamekithirisha njama zao dhidi ya msikiti wa al-Aqswa kwa kuendelea kuchimba mashimo na njia za chini kwa chini kuelekea katika msikiti huo mtakatifu ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu, hatua ambazo zinalalamikiwa vikali na Waislamu kote ulimwenguni.

Tags