Mar 02, 2021 10:42 UTC
  • Bunge la Ulaya
    Bunge la Ulaya

Wabunge wa Bunge la nchi 22 za Ulaya wameutaka Umoja wa Ulaya kuzuia mikakati ya utawala ghasibu wa Israel ya kutaka kulikalia kwa mabavu na kulitwaa eneo la Ukingo wa Magharibi huko Palestina.

Kundi la wawakilishi 442 la Bunge la Ulaya limeutaka umoja wa Ulaya kuchukua hatua zote zinazowezekana kwa ajili ya kuuzuia utawala wa Kizayuni wa Israel kulitwaa eneo la Ukingo wa Magharibi.

Wabunge hao wamesema kuwa, nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zinapaswa kutumia nyenzo zote za kidiplomasia likiwemo azimio nambari 2334 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililopasishwa mwaka 2016 ambalo linazilazimisha nchi zote duniani kutotambua rasmi vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi inayokaliwa kwa mabavu ya Palestina. 

Israel inabomoa nyumba za Wapalestina na kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni.

Utawala haramu wa Israel, ukiungwa mkono na kusaidiwa na Marekani, daima umekuwa ukipuuza maazimio na sheria za kimataifa na kuendeleza ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi ya Palestina. Sheria za kimataifa zinatambua ujenzi huo kuwa ni kinyume cha sheria.

Tarehe 23 Disemba mwaka 2016 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliutaka utawala wa Kizayuni wa Israel kusitisha mara moja na kikamilifu shughuli zote za ujenzi wa vitongoji vya walowezi katika ardhi inayokaliwa kwa mabavu ya Palestina.

Tags