Mar 03, 2021 13:47 UTC
  • Askari watatu wa Marekani wauawa Iraq katika shambulio dhidi ya kituo cha anga cha Ainul-Asad

Vyombo vya habari vyenye mfungamano na makundi ya muqawama ya Iraq vimetangaza kuwa, askari watatu wa Marekani wameuawa katika shambulio dhidi ya kituo cha anga cha Ainul-Asad kilichoko mkoani Al Anbar magharibi mwa nchi hiyo.

Kanali ya habari ya Saabirin News imetangaza kuwa afisa mmoja na askari wawili wa jeshi la Marekani wameuawa katika shambulio la maroketi lililofanywa leo dhidi ya kituo cha anga cha Ainul-Asad na kwamba maiti za watu hao zimesafirishwa kwa ndege ya kitengo cha 386 cha jeshi hilo na kupelekwa kituo cha Ali-ssaalim kilichoko nchini Kuwait kabla ya kuhamishiwa Frankfurt, Ujerumani.

Kufuatia shambulio hilo, vikosi vya jeshi la Marekani vimefunga sehemu ya shughuli za kijeshi za kituo hicho cha Ainul-Asad na kuwahamisha askari wake kupitia mnara wa ulinzi.

Shirika rasmi la habari la Iraq limethibitisha kutokea shambulio hilo la leo dhidi ya kituo hicho na kutangaza kuwa kituo cha Ainul-Asad ni makao ya askari wa Marekani na wa Iraq na kimeshambuliwa kwa makombora kumi.

Taswira ya satalaiti ya kituo cha anga cha Ainul Asad

Licha ya duru rasmi kuthibitisha shambulio hilo na idadi hiyo ya makombora, lakini kwa mujibu wa Saabirin News, makombora 14 yalifyatuliwa kulenga kituo hicho cha anga cha jeshi la kigaidi la Marekani.

Askari vamizi wa jeshi la kigaidi la Marekani wamepiga kambi nchini Iraq tangu mwaka 2003, wakati wananchi na makundi ya Kiiraqi wameshapaza sauti zao mara kadhaa kutaka askari hao waondoke katika ardhi ya nchi yao huku bunge la Iraq pia likiwa limepitisha mpango kuhusiana na kuondoka jeshi la kigaidi la Marekani nchini humo.../

Tags