Mar 04, 2021 06:25 UTC
  • Sheikh Naim Qassem
    Sheikh Naim Qassem

Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa Marekani na utawala wa kizayuni wa Israel zinajua vyema kwamba uamuzi madhubuti wa harakati hiyo wa kujibu mapigo na uchokozi wa aina yoyote hauwezi kubadilika.

Sheikh Naim Qassem amesema Hizbullah itaendelea kuwa katika hali ya kujilinda na kuongeza kuwa, Israel inapaswa kuelewa kwamba, haina uwanja wa kutamba na iwapo itafanya mashambulizi, Hizbullah itaufanya mchana wa Israel kuwa usiku. 

Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema hali ya sasa ya Lebanon ni ngumu na tata na kuongeza kuwa, pande zote zinapaswa kufanya jitihada za kuiondoa nchi hiyo katika hali ya sasa. 

Kuhusu uhusiano wa harakati ya Hizbullah na Marekani, Sheikh Naim Qassem amesema, Hizbullah haina uhusiano wa aina yoyote na Marekani kwa sababu hakuna tofauti baina ya nani anashika madaraka huko Marekani. 

Sheikh Naim Qassem

Akizungumzia msimamo wa Marekani kuhusu Saudi Arabia, Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema: Mbinu za Joe Biden za kuidhalilisha na kuidunisha Saudia zinatofautiana na zile zilizokuwa zikitumiwa na mtangulizi wake, Donald Trump, lakini wote wawili wanaamini kuwa Washington inapaswa kuishinikiza Saudi Arabia kwa shabaha ya kudhamini maslahi yake. 

Tags