Mar 22, 2021 08:18 UTC
  • Makumi wauawa na kujeruhiwa huko Halab Syria katika mashambulizi ya magaidi wanaoungwa mkono na Uturuki

Makumi ya watu wameuawa na wengine kujeruhiwa katika mashambulizi ya makombora yaliyofanywa akatika baadhi ya maeneo ya mji wa Halab huko Syria na magaidi wenye silaha wanaongwa mkono na Uturuki.

Watu wawili wameuawa na 17 wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo ya magaidi wanaoungwa mkono na Uturuki huko Syria. Afisa mmoja wa jeshi la Syria katika mkoa wa Halab ameeleza kuwa, mashambulio hayo ya magaidi wanaoungwa mkono na Uturuki yameyavilenag pia vitongoji vya Froudevin na Salehin. 

Duru za kieneo pia huko kaskazini mwa mkoa wa Halab zimeripoti kujiri mlipuko wa gari lililotegwa bomu katika makao makuu ya mkoa huo. Watu kadhaa wameuawa na kujeruhiwa katika mlipuko huo. 

Wakati huo huo Taasisi ya Kutetea Haki za Binadamu ya Syria imetangaza kuwa Uturuki juzi usiku ilifanya mashambulizi katika eneo linalodhibitiwa na wapiganaji wa Kikurdi huko kaskazini mwa Syria. 

Tags