Mar 29, 2021 04:20 UTC
  • Waziri Mkuu wa Iraq asisitiza kufanyika uchaguzi kama ilivyopangwa

Waziri Mkuu wa Iraq amesisitiza kuwa uchaguzi wa bunge nchini humo utafanyika kama ilivyopangwa yaani tarehe 10 mwezi Oktoba mwaka huu.

Mustafa al Kadhimi Waziri Mkuu wa Iraq ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa, serikali inachukua hatua kwa azma na irada kamili ili kutekeleza mipango yake licha ya upinzani na hatua za kutaka kukwamisha uchaguzi huo. 

Al Kadhimi ameashiria namna anga hasi inavyosambaratisha matarajio pekee na thamani za Wairaqi kwa ajili ya mustakbali mwema wa Iraq na kueleza kuwa, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu uchaguzi wa bunge wa nchi hiyo utafanyika kama ilivyopangwa na serikali haitarudi nyuma katika kuijenga nchi hiyo.

Mustafa al Kadhimi

 Kabla ya hapo, serikali ya Iraq ilitangaza tarehe sita mwezi Juni kuwa siku ya kufanyika uchaguzi wa mapema wa bunge hata hivyo zoezi la upigaji kura liliakhirishwa na badala yake uchaguzi huo umepangwa kufanyika tarehe 10 mwezi Oktoba mwaka huu.  

Tags