Apr 07, 2021 03:33 UTC
  • Askari wa Israel wamuua shahidi dereva wa Kipalestina Ukingo wa Magharibi

Wanajeshi katili wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamemuua shahidi dereva Mpalestina kwa kumpiga risasi akiwa ndani ya gari lake katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Wizara ya Afya ya Palestina imesema derava huyo wa Kipalestina aliyeuawa shahidi kwa jina Osama Mansour na aliyekuwa na umri wa miaka 42, aliuawa katika hali ambayo hakuwa na silaha yoyote.

Mjane wa marehemu, Sumaya Mansour ambaye alijeruhiwa vibaya kwa risasi katika tukio hilo la jana Jumanne amesema hafahamu ni kwa nini wanajeshi hao wa Israel waliwafyatulia risasi, wakati ambapo walisimamisha gari lao kama walivyoagizwa na askari hao wa Kizayuni. 

Amesema baada ya kusimamisha gari lao katika kituo cha upekuzi, wanajeshi hao wa Israel waliwatazama na kisha wakaawambia waondoke, na hapo ndipo wakaanza kuwamiminia risasi.

Wanajeshi wa Israel wakifurahi na kucheka baada ya kuwafanyia Wapalestina ukatili

Naye Salem Eid, meya wa Biddu, eneo anakotoka dereva huyo wa Kipalestina aliyeuawa shahidi amesema wanatafakari kuliwasilisha faili la mauji hayo katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC.

Mapema mwezi uliopita pia, askari wa utawala haramu wa Kizayuni waliwaua shahidi wavuvi watatu Wapalestina baada ya kuifyatulia kombora boti yao ya uvuvi, karibu na pwani ya eneo la Khan Yunes, katika Ukanda wa Gaza. Kabla ya hapo, polisi wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel waliwaua shahidi kwa kuwapiga risasi vijana wawili Wapalestina baada ya kuvamia eneo moja katika mji wa Tamra kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Tags