Apr 12, 2021 11:24 UTC
  • Mamluki wa Saudia na Imarati wapigana wao kwa wao kusini mwa Yemen

Mamluki wa kundi linalojiita Baraza la Mpito la Kusini lenye mfungamano na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) na wale wa serikali iliyojiuzulu ya Yemen wenye mfungamano na Saudi Arabia kwa mara nyingine tena wamepigana wao kwa wao huko kusini mwa Yemen.

Msemaji wa kundi la Baraza la Mpito la Kusini lenye mfungamano na Imarati Muhammad al Naqib  leo ametangaza kuwa, wapiganaji wa kundi hilo kwa mara nyingine tena wamepigana katika mkoa wa Abyan na mamluki wa serikali ya zamani ya Yemen iliyojizulu na kukimbilia Saudi Arabia.  

Shirika la habari la Yemen pia limeripoti kuwa, mapigano hayo yamejiri katika eneo Khabar al Muraqasha na kwamba yalianza baada ya mamluki wa Baraza la Mpito kuzishambulia ngome za wanamgambo wa serikali iliyojizulu ya Yemen. 

Duru za kieneo pia zimeripoti kuwa, mapigano hayo yamejiri katika eneo la pwani linalounganisha mikoa ya Aden na Abyan. 

Yemen

Siku mbili zilizopita, mamluki wa Baraza la Mpito la Kusini huko Yemen lilituma silaha na zana nyingi za kijeshi huko Khabar al Muraqasha na katika eneo la Ahwar na katika mji wa Zinjibar ili kujiandaa kukabiliana na wanangambo wa serikali ya Yemen iliyojizulu huko Abyan. 

Mapigano kati ya pande mbili hizo zinazounda muungano vamizi dhidi ya Yemen yameongezeka zaidi katika wiki mbili za karibuni na makumi ya watu wameuliwa na wengine kujeruhiwa katika mapigano hayo. 

Tags