Apr 13, 2021 11:29 UTC
  • Usafiri wa ndege katika baadhi ya viwanja vya Saudia wasitishwa kwa muda baada ya kushambuliwa na droni za Yemen

Usafiri wa ndege katika baadhi ya viwanja vya ndege nchini Saudi Arabia umesitishwa kwa masaa kadhaa kufuatia mashambulizi ya droni za jeshi la Yemen.

Televisheni ya al Itiijah ya Iraq imeripoti kuwa, usafiri wa anga katika miji kadhaa ya Saudi Arabia umesimamishwa kufuatia mashambulizi hayo tajwa ya ndege zisizo na rubani za jeshi la Yemen. 

Viwanja vya ndege vya Saudia vyashambuliwa na droni za jeshi la Yemen 

Idara za Kuongoza Ndege zimetangaza kuwa, ndege za Saudi Arabia zimesitishwa kuruka katika anga za miji ya Jeddah, Abha, al Damaam, al Sharqiya na katika akthari ya miji ya kusini mwa nchi hiyo. 

Jeshi na makundi ya kujitolea ya wananchi wa Yemen katika miezi ya karibuni yametekeleza mashambulizi mengi ya ndege zisizo na rubani (droni) nchini Saudi Arabia. Aidha inatabiriwa kuwa usitishwaji huo wa safari za ndege nchini Saudia utasababisha hasara kubwa kwa sekta ya usafiri wa anga ya nchi hiyo.