Apr 15, 2021 13:38 UTC
  • Wazayuni wana wasiwasi wa Iran kulipiza kisasi cha hujuma dhidi ya kituo cha nyuklia cha Natanz

Waziri mkuu wa zamani wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel amesema, ana wasiwasi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuchukua hatua ya kulipiza kisasi kwa sababu ya Israel kufanya hujuma katika kituo cha nyukulia cha Natanz.

Ehud Olmet amesema hayo leo katika mahojiano na kituo cha redio cha WABC, ambapo mbali na kukwepa kubeba dhima utawala wa Kizayuni ya kuhusika na hujuma ya Natanz, ameigeukia serikali ya Marekani inayoongozwa na Joe Biden kuitaka iudhaminie utawala wa Kizayuni usalama wake katika kukabiliana na vitisho vya viongozi wa Iran; na akasema ana uhakika Biden anazingatia usalama wa Israel.

Siku ya Jumapili, mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran, Behrouz Kamalvand alitangaza kutokea mkasa katika sehemu ya usambazaji umeme ya kituo cha nyuklia cha kurutubisha urani cha Natanz.

Ehud Olmet

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Saaed Khatibzadeh amesisitiza kuwa, Iran italipiza kisasi kwa utawala wa Kizayuni katika mahali na wakati itakaoamua na akaongeza kuwa, mashinepewa zilizoondolewa baada ya hujuma dhidi ya kituo cha Natanz zilikuwa aina ya IR1 na zitabadilishwa kwa mashinepewa za kisasa kabisa.

Siku ya Jumatatu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif alitilia mkazo udharura wa kuvilinda kwa namna inayostahiki vituo na wanasaynasi wa nyuklia katika hali hasasi na nyeti ya hivi sasa na akaongeza kuwa, Wazayuni watapata jibu lao katika maendeleo makubwa zaidi itakayopata Iran katika nyuklia.

Huko nyuma pia, kituo cha nyuklia cha Natanz kilishambuliwa kupitia hujuma za pamoja za intaneti zilizofanywa na Marekani na Israel.../ 

Tags