Apr 21, 2021 02:29 UTC
  • Arab League: Maazimio ya Baraza la Usalama la UN kuhusu ulazima kuondoka maghasibu huko Palestina yatekelezwe

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) amesisitiza udharura wa kutekelezwa maazimio yote ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yanayotaka kukomeshwa uvamizi wa Israel na kukaliwa kwa mabavu ardhi ya Palestina.

Ahmed Aboul Gheit pia amepinga ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni unaofanywa na Israel katika ardhi inayokaliwa kwa mabavu ya Palestina.

Ujenzi huo wa vitongoji vya walowezi katika ardhi ya Palestina unakiuka azimio nambari 2334 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. 

Desemba 23, 2016 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio 2334 ambalo liliutaka utawala haramu wa Israel usimamishe haraka na kikamilifu shughuli zote za ujenzi wa vitongoji katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu.

Utawala wa Kizayuni ambao unaungwa mkono kikamilifu na Marekani katika hatua zake hizo haramu umedhamiria kubadilisha muundo wa kijiografia na kidemografia wa maeneo ya Palestina; ili kwa kuyazayunisha maeneo hayo, kuhakikisha unazihodhi na kuzidhibiti kikamilifu ardhi za Wapalestina.

Tags