Apr 27, 2021 03:28 UTC
  • Zarif asisitiza kuhusu udharura wa umoja wa umma wa Kiislamu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuhusu udharura wa umoja wa umma wa Kiislamu.

Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aliyasema hayo jana mjini Baghadad Iraq wakati alipokutana na Khamis Khanjar mkurugenzi wa Taasisi ya 'Mashroo al-Arabi' pamoja na wabunge wa Ahul Sunna na pia shakhsia wengine wa Ahlul Sunna. 

Katika kikao hicho, Zarif amebainisha kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapinga ukabila na inasisitiza kuhusu umoja wa jamii ya Kiislamu.

Zarif pia amefafanua kuhusu nafasi ya Quds Tukufu katika sera za kigeni za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuongeza kuwa Iran inaunga mkono harakati za ukombozi wa Palestina na Quds Tukufu pamoja na kuwa inashinikizwa sana kutokana na msimamo wake huo. Amesema taifa la Iran linasimama bega kwa bega na Waislamu duniani katika masuala mbali mbali.

Hali kadhalika amesema kuna haja ya kuwepo uhusiano wa kimantiki baina ya kaumu mbali mbali za Iraq na kuongeza kuwa, Iran inaheshimu uwepo wa mirengo mbali mbali na madhehebu mbali mbali nchini Iraq.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran akiwa na viongozi wa kisiasa na wasomi wa Ahul Sunna nchini Iraq

Katika kikao hicho, Khamis Khanjar mkurugenzi wa Taasisi ya 'Mashroo al-Arabi' na wanachama wengine wa taasisi hiyo walioshiriki katika kikao hicho walibainisha mitazamo yao kwa kirefu kuhusu masuala ya Iraq.

Zarif aliwasili Baghdad Jumatatu kwa lengo la kufanya mazungumzo na maafisa wa ngazi za juu wa Iraq na pia kukutana na wakuu wa mashirika mbali mbali ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali.

Tayari Zarif ameshakutana na kufanya mazungumzo na mwenzake wa Iraq Fuad Hussein pamoja na Rais wa Iraq Barham Salih na waziri mkuu wa nchi hiyo Mustafa Al-Kadhimi.

 

Tags