May 01, 2021 08:00 UTC
  • Ehud Olmert: Kuna uwezekano wa kutokea Intifadha mpya ya Wapalestina

Ehud Olmert, Waziri Mkuu wa zamani wa utawala haramu wa Israel ametahadharisha juu ya uwezekano wa kutokea Intifadha mpya ya Wapalestina.

Olmert amesema kuwa, kuna mambo ambayo yametokea huko Palestina ambayo yanaandaa uwanja na mazingira ya kutokea Intifadha mpya katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu.

Kuhusiana na kuendelea mashambulio dhidi ya wananchi wa Palestina na kuwadhuru wananchi hao kwa makusudi,  Waziri Mkuu huyo wa zamani wa utawala haramu wa Israel amesema kuwa, matukio hayo kwa hakika hayawabakishii Wapalestina chaguo jingine kwa ghairi ya mapambano na Intifadha.

Ehud Olmert, Waziri Mkuu wa zamani wa utawala haramu wa Israel

 

Aidha amesisitiza kuwa, matukio ya hivi karibuni huko Baytul-Muqaddas ni ishara za wazi za Intifadha na hali mambo yumkini wakati wowote ikazidi kuwa mbaya.

Kuanza mwezi mtukufu wa Ramadhani kulikwenda sambamba na kuongezeka idadi kubwa ya Wapalestina Waislamu waliokuwa na nia ya kufanya itikafu katika msikiti wa al-Aqswa.

Hata hivyo Wapalestina hao walikabiliwa na vizingiti vya jeshi la utawala haramu wa Israel lililokuwa likiwazuia kwenda katika msikiti huo kwa ajili ya kutekeleza ibada.

Tangu wakati huo hadi sasa kumeshuhudiwa mapigano huko Quds baina ya Wapalestina na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Makundi mbalimbali ya mapambano huko Palestina ikiwemo Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina imetoa mwito wa kufanyika Intifadha ya Quds.

Tags